Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA NYWELE KUWASHA,CHANZO NA TIBA YAKE

TATIZO LA NYWELE KUWASHA,CHANZO NA TIBA YAKE

Watu wengi hupatwa na shida hii ya nywele za kichwani kuwasha sana hasa WANAWAKE,ambao husuka na kutumia mitindo mbali mbali ya Nywele.

Je unajua kwamba kuna vyanzo vingi vya shida hii,na kwa namna moja au nyingine huweza kuwa ugonjwa kabsa ambao unahitaji Tiba? Soma hapa chini kujua

CHANZO NA TIBA YA TATIZO LA NYWELE KUWASHA

– Shida hii huweza kuanzia kwenye fuvu la kichwa yaani Scalp na kwenye Vishina vya nywele zako yaani Follices,ndipo matokeo hupanda mpaka juu ya nywele na kichwa kwa ujumla, Chanzo cha tatizo la Nywele kuwasha ni pamoja na;

1. Shida ya Mba, Unga au ukurutu ambao hutoka kichwani, na hii hutokea sana kwa watu wanaopenda kuacha nywele ndefu sana au kusuka mitindo mbali mbali ya nywele(WADADA),

2. Tatizo la fangasi wa kichwani, Hapa tunazungumzia jamii ya fangasi kama Tinea Capitis ambao kwa asilimia kubwa hupenda kushambulia eneo la kichwani yani kwenye Scalp, Ringworms n.k

TIBA: Kwa mtu mwenye shida hii huweza kutumia Antifungal medications mbali mbali,

3. Shida ya Dandruff na Seborrheic dermatitis, Ambapo kinga yako ya mwili hutoa majibu yaani Inflammatory response,

Na hii ni baada ya kuwa na kiwango kikubwa sana cha Maambukizi ya YEAST(yeast overgrowth), hali ambayo husababisha tatizo la mtu kuwashwa kichwani,

TIBA: Kama tatizo sio kubwa sana mtu huweza kutumia shampoos ambazo zina Selenium au Zinc pyrithionic na shida hyo ikaisha kabsa, Ila kama tatizo ni kubwa zaidi,mtu huweza kutumia Antifungal shampoos,Topical cortisone,Cream,Ointment n.k

4. Tatizo la Psoriasis, Hili ni tatizo ambalo ni chronic autoimmune disease,ambapo huweza kuleta madhara mbali mbali kama vile Hali ya wekundu sana kwenye ngozi ya kichwani,Miwasho,vidonda n.k

TIBA: Kama tatizo sio kubwa sana,Mgonjwa huweza kutumia Shampoo zenye Coal Tar au Salicylic Acid

5. Tatizo la chawa wa Kichwani(Head LICE),Baadhi ya watu hufikiria shida hii hutokea kwa watoto tu washuleni,watu wachafu n.k, Ila ukweli ni kwamba chawa hawa huweza kushambulia mtu yoyote,

TIBA: Kama tatizo sio kubwa sana,tumia shampoos za kichwani zenye Insecticides pyrethrin au Permethrin

6. Shida ya Mzio au Allergic reaction, Shida hii ya allergy huweza kutokana na sababu mbali mbali kama vile; Matumizi ya baadhi ya aina za Dawa za nywele, shida ya Eczema au Atopic Dermatitis,

TIBA: Tumia anti allergy medications kutibu shida hii,

KUMBUKA; Tafta msaada zaidi kwa Wataalam wa Afya endapo;

– Umetumia shampoos kama hizo hapo juu ila bado shida ipo

– Unapata miwasho sana Wakati wa usku hadi unakosa usingizi

– Unapata miwasho sana mpaka unashindwa kufanya kazi zako

– Unaona kabsa Chawa(Lice) kwenye kichwa chako

– Umeanza kupata vidonda kichwani kwako

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.