Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA MWANAMKE KUKOSA HISIA,CHANZO CHAKE

TATIZO LA MWANAMKE KUKOSA HISIA,CHANZO CHAKE

Tatizo hili la mwanamke kukosa hisia au hamu ya tendo la ndoa,huwapata wanawake wengi kwa hivi sasa, huku wengine wakipata pia matatizo mengine kama vile; kushindwa kuridhika au kufika kileleni(orgasm), kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa n.k.

CHANZO CHA TATIZO LA MWANAMKE KUKOSA HISIA

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mwanamke kukosa hisia au hamu ya kufanya tendo la ndoa. Na sababu hizo ni kama vile;

– Matatizo anayoyapata wakati wa tendo la ndoa, kama vile kupata maumivu makali wakati wa tendo pamoja na kutokufika kileleni(orgasm),

sababu hizi huweza kusababisha mwanamke akakosa kabsa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

– Magonjwa kama vile: arthritis, Kansa, ugonjwa wa kisukari, presha, magonjwa ya moyo kama vile coronary artery disease, neurogolical diseases n.k

magonjwa yote haya huweza kusababisha mwanamke akose kabsa hisia au hamu ya tendo la ndoa.

– Matumizi ya dawa mbali mbali kama vile dawa jamii ya antidepressants n.k

– Matumizi ya Pombe kupita kiasi,uvutaji wa sigara pamoja na vilevyi vingine, vyote hivi huweza kusababisha hamu ya tendo la ndoa kupotea.

– Upasuaji, hasa kwa Wanawake ambao wamefanyiwa upasuaji wa matiti pamoja na sehemu zao za siri, hii inaweza kuathiri pia hamu ya tendo la ndoa

– Uchovu, mwili ukiwa umechoka kupita kiasi, mfano kutokana na kazi nyingi sana, inaweza kusababisha mwanamke kukosa hisia au hamu ya tendo

– Mabadiliko ya vichocheo mwilini(hormones changes) kutokana na sababu mbali mbali kama vile;

• Mwanamke kufikia kipindi cha ukomo wa hedhi yaani Menopause, ambapo hutokea mabadiliko makubwa ya vichocheo mwili ikiwemo kichocheo cha ESTROGEN, ambapo level ya estrogen hushuka sana kipindi hiki hali ambao huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu,uke kuwa mkavu n.k

• Ujauzito pamoja na unyonyeshaji(pregnancy and breastfeeding), mwanamke kupata mabadiliko makubwa sana ya vichocheo mwilini katika vipindi hivi viwili yaani kipindi cha ujauzito pamoja na kipindi cha unyonyeshaji,

hali ambayo hupelekea baadhi ya Wanawake kupoteza kabsa HAMU ya Tendo la Ndoa.

• Matumizi ya njia za uzazi wa mpango kama vile vidonge,sindano n.k huweza pia kupelekea mabadiliko ya vichocheo mwilini

– Sababu nyingine ni pamoja na matatizo ya kisaikolojia ambayo huchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;

✓ Hofu,wasiwasi, huzuni,msongo wa mawazo n.k

✓ Ugomvi wa kimahusiano n.k

✓ Kupata maumivu kwenye tendo la ndoa kwa sku za hapo nyuma, huweza kusababisha mwanamke kuogopa,kupata hofu ya kurudia tendo pamoja na kupoteza hamu ya tendo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.