Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Saratani ya Uume,Chanzo,Dalili na Tiba yake

Saratani ya Uume,Chanzo,Dalili na Tiba yake

Kansa au Saratani ya UUME, huhusisha seli kukua bila kudhibitiwa kwenye uume wa mwanaume.

Kuna aina Mbali mbali za Saratani/Kansa ya Uume kama vile;

1.Squamous cell au epidermoid carcinoma.Hii huchukua Asilimja 95% ya kesi za saratani ya uume. Kawaida huanza juu au chini ya govi lako lakini pia inaweza kuonekana kwenye sehemu zingine za uume wako

2.Sarcoma. Aina hii ya Kansa ya Uume hutokea kwenye tissue mbali mbali kama vile kwenye mishipa ya damu,misuli,n.k

CHANZO CHA KANSA AU SARATANI YA UUME

Wataalamu wa afya hawajui nini hasa husababisha saratani ya uume. Utafiti unaonyesha kuwa Tatizo hili hutokea zaidi kwa wanaume ambao;

– Wana virusi aina ya human papillomavirus (HPV)

– Wenye umri wa zaidi ya miaka 60

– Wanaovuta Sigara

– Wenye Kinga ya Mwili Dhaifu kutokana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI

– Wanaume ambao hawajatahiriwa,Vimiminika na mkusanyiko mwingi unaoitwa smegma unaweza kukusanywa chini ya govi lako na kuweza kupelekea ukuaji wa saratani.

– mwanaume kuwa na hali inayoitwa phimosis, ambayo hufanya govi lako kuwa gumu na kukaza, hali ambayo husababisha iwe vigumu kulisafisha. Inaweza pia kusababisha mkusanyiko wa maji. N.k

DALILI ZA KANSA AU SARATANI YA UUME

Mabadiliko katika ngozi ya uume ndio dalili inayojulikana zaidi ya saratani ya uume. Inaweza kuonekana kwenye govi la wanaume wasiotahiriwa, kwenye ncha ya uume (glans), au kwenye shimo.

Dalili za saratani ya uume ni pamoja na:

• Mabadiliko katika unene wa ngozi au rangi

• Upele au matuta madogo kwenye uume wako; inaweza kuonekana kama kigaga ambacho hakijapona.

• Ukuaji unaoonekana hudhurungi-hudhurungi

• Kivimbe kwenye uume wako

• Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya chini ya govi lako

• Kidonda kwenye uume wako, ambacho kinaweza kuvuja damu

• Kuvimba mwishoni mwa uume wako

• Uvimbe chini ya ngozi ya Uume wako n.k

Ishara hizi hazimaanishi saratani ya uume kila wakati. Unaweza kuwa na maambukizi mengine au mzio(allergy). Lakini ni muhimu kumwambia daktari wako kuhusu dalili zozote zisizo za kawaida kwenye au karibu na uume wako mara moja.

VIPIMO AMBAVYO HUWEZA KUFANYIKA NI PAMOJA NA;

– Kuchukua biopsy,Kuchukua kinyama kidogo kama sehemu ya Tissue kwenye ngozi ya Uume,

– Kufanya kipimo cha X-rays, CT scans, ultrasounds,magnetic resonance imaging (MRI) n.k

MATIBABU YA KANSA AU SARATANI YA UUME

Kama kansa Imegundulika Mapema, kwenye hatua za mwanzoni kabsa, Mgonjwa huweza kupata dawa kwenye mfumo wa Cream za kupaka,Upasuaji wa Kuondoa Sehemu iliyoathirika,Mwanaume kutahiriwa kama hajatahiriwa,

Pamoja na Tiba Zingine kama Vile:

– Huduma ya Cryotherapy,

– Huduma ya Radiation,chemotherapy n.k

ZINGATIA MAMBO HAYA: KWA WANAUME;

Hakuna njia moja ya kuzuia saratani, lakini mambo kadhaa yanaweza kupunguza hatari kwako:

1. Hakikisha Mwanaume Unatahiriwa, Wakati huna govi, ni rahisi kuweka eneo hili safi.

2. Hakikisha Usafi wa Sehemu Za Siri ikiwemo Nguo zako za Ndani

3. Usitumie tumbaku, wala Kuvuta Sigara ya Aina yoyote

4. Epuka Ngono Zembe ili kujikinga na maambukizi ya HPV na VVU.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.