Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kupumua kwa shida,chanzo chake na Matibabu yake

Kupumua kwa shida,chanzo chake na Matibabu yake

Katika Makala hii tunachambua zaidi kuhusu chanzo cha tatizo la Kupumua kwa shida,Pamoja na Matibabu yake,Soma hapa kwenye makala hii.

Kupumua kwa shida

Dyspnea ni tatizo linalohusisha mtu Kupumua kwa shida, na huweza kuwa kiashiria cha matatizo mbali mbali ya kiafya ambayo asilimia kubwa huathiri mfumo wa upumuaji(respiratory system),ingawa wakati mwingine sio tatizo ambalo huhitaji matibabu,

Tatizo la Kupumua kwa shida huweza kutokea gafla, kuwa la muda mfupi na kwa kiwango kidogo,

au kuwa la muda mrefu na hatari zaidi, Hii ni kutegemea na chanzo husika cha tatizo la Kupumua kwa shida.

Chanzo cha Tatizo la Kupumua kwa shida

Zipo sababu mbali mbali za mtu kupata tatizo la Kupumua kwa shida ikiwemo;

– Kupumua kwa shida baada ya kufanya mazoezi kupita kiasi(Intense exercise)

– Kupumua kwa shida baada ya kupanda maeneo ya muinuko zaidi kama vile milimani n.k

Hizo ni sababu za kawaida zinazoweza kupelekea mtu Kupumua kwa shida,ambapo sio kwamba unatatizo lolote la kiafya na wala huhitaji matababu zaidi.

Ingawa Zipo Sababu zinazopelekea tatizo la Kupumua kwa shida ambazo zinaashiria tatizo flani kiafya,Sababu hizo ni pamoja na;

– Ugonjwa wa Pumu au asthma

– Tatizo la kuwa na wasiwasi kupita kiasi-anxiety disorder

– Kuwa na tatizo la pneumonia

– Kuwa na magonjwa mbali mbali ya Moyo

– Kuingiwa na kitu kisha kuziba njia ya hewa, hii pia huweza kusababisha mtu Kupumua kwa shida

– Kuwa na tatizo la Mzio(allergic reactions).

– Kuwa na tatizo la Upungufu mkubwa wa damu mwilini(anemia)

– Kuwa kwenye mazingira yenye kiwango kikubwa cha carbon monoxide,

mfano; kwa wale ambao hujisahau na kulala ndani na jiko la mkaa linalowaka huku wakifunga milango na madirisha, hii ni hatari sana na huweza kusababisha kifo,baada ya mkusanyiko mkubwa wa hewa hii chafu ndani ya nyumba.

– Kuwa na tatizo la moyo kushindwa kufanya kazi(heart failure), hii pia huweza kusababisha tatizo la Kupumua kwa shida

– Presha ya damu kushuka yaani hypotension

– Kuwa na tatizo la pulmonary embolism, pamoja na matatizo mengine kwenye mapafu kama vile collapsed lung n.k

– Kuwa na tatizo la chronic obstructive pulmonary disease (COPD)

– Kuwa na matatizo mbali mbali ya moyo kama vile;

  • pericarditis
  • cardiomyopathy n.k

– Pia kuwa na tatizo la Uzito kupita kiasi au unene(overweight/obesity/) huweza kuchangia mtu kupata tatizo la Kupumua kwa shida mara kwa mara

– Kuwa na matatizo mbali mbali yanayoathiri mapafu kama vile;

  • Kupata ajali au kuumia eneo la Mapafu
  • Kuwa na Saratani ya Mapafu(Lung cancer)
  • Kuwa na ugonjwa wa Tb(tuberculosis)
  • Kuwa na tatizo la pleurisy,
  • Kuwa na tatizo la pulmonary edema,
  • Kuwa na tatizo la pulmonary hypertension,
  • sarcoidosis, n.k

Vyote hivi huweza kusababisha tatizo la Kupumua kwa shida.

– Sababu zingine zinazoongeza hatari ya kupata tatizo la Kupumua kwa shida ni pamoja na;

  • Uvutaji wa Sigara
  • Kuvuta kemikali kwa njia ya hewa
  • Kufanya kazi au kuishi maeneo ya vumbi sana n.k

Hakikisha unaonana na wataalam wa afya,endapo unapata tatizo la Kupumua kwa shida,ili kufanya vipimo na kupata matibabu Zaidi.

Vipimo kwa mtu mwenye tatizo la Kupumua kwa shida

vipimo mbali mbali huweza kufanyika kwa mtu mwenye tatizo la Kupumua kwa shida ikiwemo;

  • X-ray scans/chest X-rays
  •  CT scans
  • Electrocardiograms:
  • Spirometry tests:  n.k

Matibabu ya tatizo la Kupumua kwa shida

Matibabu ya tatizo la Kupumua kwa shida hutegemea na chanzo chake,

mfano kama chanzo ni asthma,basi mgonjwa ataanza matibabu ya asthma, n.k

Zingatia haya kama una tatizo la Kupumua kwa shida

✓ Epuka uvutaji wa Sigara

✓ Epuka kuishi au kufanya kazi sehemu za vumbi sana

✓ Epuka Kuwa kwenye mazingira yenye kiwango kikubwa cha carbon monoxide,

✓ Fanya mazoezi ya kuimarisha moyo pamoja na mfumo mzima wa upumuaji yaani cardiovascular and respiratory systems,

lakini kumbuka kufanya mazoezi kwa kiasi.

✓ Hakikisha unaonana na wataalam wa afya kama unapata tatizo la Kupumua kwa Shida.

AU KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.