Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Faida za kunyonyesha mtoto miezi sita,Soma hapa(UNYONYESHAJI)

Faida za kunyonyesha mtoto miezi sita,Soma hapa(UNYONYESHAJI)

kuna faida kubwa kwa Mama kumnyonyesha mtoto maziwa yake pekee kwa miezi 6 bila kumchanganyia na kitu kingine,

Hii kwa kitaalam hujulikana kama exclusive breastfeeding.

Kunyonyesha kuna faida nyingi sana kwa mtoto mchanga pia na kwa mama. Tuanze na faida kwa mtoto:

Faida za kunyonyesha mtoto miezi sita

1. Mtoto kupata Virutubisho vyote muhimu vya kumuwezesha kukua vizuri

Hapa tunazungumzia virutubisho kama vile;

  • vitamin,
  • protini,
  • na mafuta mazuri

Virutubisho vilivyomo kwenye maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto mchanga , fahamu maziwa ya mama huwa na uwiano mzuri wa virutubisho kama vile vitamin, protini, na mafuta mazuri na kumuwezesha mtoto kukuwa vizuri.

2. Ulinzi dhidi ya magonjwa mbali mbali,

Vilevile maziwa ya mama huwa na virutubisho vyenye uwezo wa kumkinga mtoto kupata magonjwa, kitaalamu ‘antibodies’, ambavyo humkinga mtoto mchanga dhidi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile bakteria na virusi.

3. Maziwa ya mama hupunguza uwezekano wa mtoto mchanga kupata tatizo la pumu pamoja na aleji

4. Na vilevile watoto wakinyonyeshwa kwa miezi sita mfululizo bila kuchanganyiwa na vyakula vingine hupunguza hatari ya kupata maambukizi ya masikio, mfumo wa hewa na magonjwa ya kuharisha.

Hizo ni baadhi ya Faida za kunyonyesha mtoto miezi sita.

Faida za kunyonyesha kwa mama

Faida za kunyonyesha kwa mama ni kama zifuatazo:

-Husaidia kupunguza uzito kwa mama hasa baada ya kujifungua

-Husaidia kutolewa kwa kichochezi cha Oxytocin ambacho husaidia kurudisha mfuko wa kizazi katika size yake ya zamani kabla ya ujauzito

-Husaidia kupunguza hatari ya saratani za matiti na ovary, pia hupunguza hatari za matatizo ya mifupa

-Husaidia Mama kuwa karibu na mtoto (bonding)

Inashauriwa Mama kumnyonyesha mtoto pale anapohisi kuwa ana njaa. Wengi wamekuwa wakitegemea kumsikia mtoto analia kama ishara ya njaa, lakini kulia ni ishara ya mwisho ya njaa, ina maana mpaka analia itakuwa ameshasikia njaa na ameshindwa kuvumilia.

Ishara kuwa mtoto ana njaa (anahitaji kunyonyeshwa)

Zifuatazo ni baadhi ya ishara kuwa mtoto ana njaa (anahitaji kunyonyeshwa)

-Anazungusha kichwa huku na huku

-Anaachama mdomo

-Anang’atang’ata ulimi kama anamung’unya kitu

-Anakula vidole

-Analamba midomo

-Anajaribu kushikashika vitu

-Ishara nyingine hutegemeana na mtoto, hivyo kama mama, unatakiwa uhakikishe umezizoea na kujua ishara kuu za mtoto wako.

Ninajuaje kama mtoto hapati maziwa ya kutosha?

Swali hili ni moja ya maswali ambayo wamama wengi wamekuwa wakijiuliza, je nitajuaje kama mtoto anapata maziwa ya kutosha,

Zifuatazo ni baadhi ya ishara kuonyesha kuwa mtoto hapati maziwa ya kutosha;

-Unamuona anakuwa hajatosheka hata baada ya kunyonya

-Anakuwa na njaa kwa vipindi vifupivifupi sana

-Anapata choo au mkojo mara chache saaana

-Ana hasira na ana lialia sana

-Haongezeki uzito

Endapo utaona dalili hizi, zingatia kwenda hospitali au wasiliana na wataalam wa afya kwa ushauri zaidi ili kuweza kupata suluhisho.

Sababu kuu za maziwa kulala

Ni muhimu kufahamu, Unyonyeshaji hauchangii maziwa kulala wala kuharibu umbo la maziwa,

Sababu kuu za maziwa kulala ni pamoja na;

1️⃣Umri

2️⃣Vinasaba vya urithi

3️⃣Unene wako wa mwili

4️⃣Utapiamlo hasa ukiwa na upungufu wa vitamin C

5️⃣Kuvuta sigara

6️⃣Kujifungua mara nyingi n.k

Kuhusu kubeba ujauzito mara nyingi, Mama anapokuwa mjamzito maziwa hupitia mabadiliko kama kuongezeka ukubwa na umbo,

Baada ya kujifungua umbo hurudi lilivyokuwa kabla lakini huwa tofauti kidogo. Mabadiliko haya hutokea kila ujauzito, mwisho maziwa hulala na sio kwasababu ya kunyonyesha.

Vitamin C hutengeneza Collagen,malighafi muhimu kwenye ngozi na kiwambo kinachoshika maziwa.

Iwapo mwanamke hapati Vitamin C ya kutosha ngozi na kiwambo cha maziwa huwa dhaifu na maziwa hulala.

Vitamin C hupatikana Kwa wingi kwenye machugwa, chenza, viazi lishe n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.