Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

kuzaa mapacha,jinsi ya kuzaa watoto mapacha

kuzaa mapacha,jinsi ya kuzaa watoto mapacha

JINSI YA KUPATA WATOTO MAPACHA (TWINS)

☑️SUMMARY

Tutajadili kwa kina katika vipengele vifuatavyo ?
(1) Maana ya Mapacha ambao kitaalam hujulikana  kama TWINS
(2) Aina za Mapacha ambazo ni mbili Mapacha wanaofanana(Identical Twins) na mapacha wasiofanana(Fraternal Twins)
(3) Jinsi mapacha hawa wanavyotokea kwa aina zote hizi mbili
(4) Jinsi ya Kugundua kama Una mapacha Tumboni
(5) Maelekezo mwishoni kama unahitaji Ushauri,Elimu au tiba kwa Tatizo lolote la kiafya

Watoto mapacha ni nini?

•Watoto mapacha (TWINS)- ni watoto wawili ambao wanazaliwa wakati mama anajifungua, ambapo wanaweza kuwa watoto wa jinsia moja yaani wanawake Wote au wanaume wote,au wakawa wa jinsia tofauti yaani mwanamke na mwanaume.

AINA ZA MAPACHA

Kuna aina mbili za mapacha,nazo ni kama ifautavyo;

(1) Mapacha wanaofanana au kitaalam huitwa Identical Twins- mapacha hawa kama lilivyo jina lao kwa asilimia kubwa hufanana vitu vingi mfano Group lao la Damu, Jinsia- kama ni wakike wote wanakuwa wakike na kama ni wakiume wote basi wanakuwa wakiume

(2) Mapacha wasiofanana au kitaalam huitwa Fraternal Twins- na hawa kama lilivyo jina lao kwa asilimia kubwa wanakuwa na vitu vinatofautiana Mfano Jinsia kama mmoja ni wakike mwingine ni wakiume,group lao la damu n.k

JINSI MAPACHA HAWA WANAVYOTOKEA

kwanza tuwekane sawa hapa; Ili Ujauzito utokee lazima mbegu ya mwanaume iweze kulikuta Yai linalotoka katika vifuko vya Mayai vya mwanamke yaani OVARIES,ifanikiwe kuingia ndani na kulirutubisha Yai hilo,ambapo kwa asilimia kubwa urutubishaji huo hutokea katika mirija ya uzazi yaani Fallopian Tubes, Hapo ndipo ujauzito hutokea na safari ya mtoto kuzaliwa huanzia hapo.

(A) Mapacha wanaofanana au Identical Twins jinsi wanavyotokea- Mbegu moja ya mwanaume kufanikiwa kulikuta yai moja la mwanamke,kuingia ndani na kulirutubisha,ambapo baada ya urutubishaji lile yai hugawanyika mara mbili,hapo ndipo mapacha wanaofanana hutokea.

(B) Mapacha wasiofanana au Fraternal Twins- Aina hii ya mapacha(Twins) hutokea pale ambapo mbegu mbili za mwanaume zimefanikiwa kuyakuta mayai mawili kutoka katika vifuko vya mayai ya mwanamke yaani OVARIES,kuingia ndani, na kuyarutubisha hayo mayai mawili,Hapa ndipo watoto mapacha wasio fanana hutokea au Kitaalam tunasema Fraternal Twins.

JINSI YA KUGUNDUA KAMA UNA MAPACHA

✓Kipimo cha Ultrasound, kipimo hiki husaidia kujua kama mjamzito ana watoto mapacha au mtoto mmoja tumboni

✓Kupimwa na wataalam wa afya kwa kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto tumboni kwa kutumia kifaa maalum kijulikanacho kama FETOLSCOPE

✓Mjamzito kuwa na tumbo kubwa kupita kiasi,Japo sio kila tumbo kubwa basi ni watoto mapacha,wengine ni matatizo kama,Tatizo la Big baby(Mtoto mkubwa sana tumboni), Tatizo la kujaa maji ya uzazi na matatizo mengine kama hayo

✓Mama anapojifungua,hapo ndyo ukwel wa mambo yote utajulikana, kwamba je mtoto ni mmoja au ni mapacha

Kumbuka; Watoto wakiwa watatu sio TWINS tena bali huitwa TRIPLETS, na uwezekano wa kuzaa watoto mapacha ni mkubwa kuliko uwezekano wa kuzaa watoto watatu kwa wakati mmoja

 VITU VYA KUZINGATIA ILI MTOTO AWE NA AFYA BORA

(1)Lishe au anachokula mtoto wako,Mfano mtoto anapozaliwa tu anatakiwa kupewa maziwa ya mama yake pekee bila kuchanganyiwa na kitu chochote mpaka afikishe umri wa miezi sita kitaalam huitwa EXCLUSIVE BREASTFEEDING, baada ya hapo Ndipo apewe maziwa ya mama au anyonyeshwe pamoja na kuchanganyiwa vyakula vingine mpaka atapofikisha umri wa miaka 2 au 3.Kwahyo basi kiufupi mtoto huyo anatakiwa kunyonya mpaka umri wa miaka miwili mpka mitatu
(2)Chanjo- Kuna chanjo za Muhim sana kwa mtoto lazima azipate kuanzia anapozaliwa mpka atakapofikisha umri wa miaka mitano.Mfano;
-Chanjo ya begani kwa ajili ya kuzuia kifua kikuu(BCG)
-Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza yaani POLIO
-Chanjo ya kuzuia Ugonjwa wa kuharisha yaani ROTARIX
-Dawa za  minyoo
-Vitamin A
-Chanjo ya kuzuia magonja kama,Kifaduro,homa ya manjano,homa ya Ini, n.k kitaalam huitwa PENTAVALENT VACCINE- mana ake hii huzuia magonjwa matano.
(3)Usafi kwa mtoto ni kitu cha muhimu sana kwake pia
(4)Kitovu cha mtoto kisiwekwe kitu chochote mpaka kidondoke chenyewe
Imani potofu kama kuweka Mavi ya Ng’ombe kwenye kitovu cha mtoto huweza kuleta magonjwa kwa mtoto
(5)Endapo kitovu kinavuja damu,mpeleke mtoto hospital kwa,wataalam wa afya
(6)Zijue dalili za hatari kwa mtoto,mfano mtoto kubalika rangi na kuwa manjano,mtoto kushindwa kunyonya,mtoto kupata homa,degedege,mtoto kulia tu mda wote n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.