Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Rais wa Ngumi Tanzania Atoa Ufafanuzi ‘Mandonga Hajafungiwa Kucheza Ngumi’

Rais wa Kamisheni inayosimamia ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) Chaulembo Palasa ameiambia @AyoTV_ kuwa Bondia Mtanzania Karim Mandonga hajafungiwa kama inavyoripotiwa na baadhi ya Vyombo vya Habari bali sheria za ngumi nchini zinamtaka Bondia yoyote atayepoteza pambano kwa KO au TKO kabla ya kurudi ulingoni kwa pambano jingine kupimwa afya.

Palasa mesema kwakuwa Mandonga alipoteza dhidi ya Moses Golola Raia wa Uganda July 29 2023 Jijini Mwanza kwa TKO haruhusiwi kupanda ulingoni kucheza pambano jingine hadi afanyiwe vipimo vya afya kwa usalama wake.

Hivyo Mandonga jana amefanyiwa vipimo vya afya (MRI ya kichwa) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na majibu yatatoka leo August 15, 2023 saa 9:00 Alasiri kama yupo sawa kiafya kurejea ulingoni kwani ana pambano Zanzibar August 27,2023.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.