Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Vyakula Rafiki Kwa Wagonjwa Wa Figo

VYAKULA RAFIKI KWA WAGONJWA WA FIGO

Ugonjwa wa figo ni moja ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo pamoja na sababu nyingine yanayohusiana pia na ulaji usiofaa na mtindo ya maisha.

Vyakula Bora kwa Mgonjwa wa Figo;

Ni pamoja na vyakula vya protini nyepesi na nafaka zisizokobolewa. Mboga za majani na matunda.

Mgonjwa anatakiwa kudhibiti ulaji wake kwa kufanya mabadiliko ya aidha kupunguza kiasi au kuacha kula aina fulani ya vyakula.

Vyakula hivi vinaweza kutumiwa na wagonjwa wa figo ili kuwawezesha kuimarika kila siku:

(1) Kabeji iliyopikwa

Kabeji ni miongoni mwa mbogamboga ambazo hazina madini ya potasiamu kwa kiasi kikubwa ambayo ni hatari kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo.

Katika kundi la mbogamboga, mgonjwa wa figo anashauriwa kula kabeji kwa wingi.

(2) Vyakula vingine vyenye kiasi kidogo cha potasiamu ni pamoja na jamii ya

  • maharage mabichi au kutumia (green beans),
  • karoti iliyopikwa,
  • mahindi mabichi,
  •  tango,
  • bilinganya,
  • kitunguu,
  • giligilani,
  •  njegere,
  •  pilipili mbichi
  •  Pamoja na spinachi mbichi.

KUMBUKA:Mwili wa mgonjwa wa figo haupaswi kupata vyakula vyenye madini ya potasiamu kwa wingi kama parachichi, ndizi, nazi, embe, chungwa, peasi, komamanga, tende, viazi vikuu, viazi vitamu, viazi ulaya, na matunda yaliyokaushwa.

“Ni rahisi sana kwa mgonjwa wa figo kulundika kiasi kikubwa cha potasiumu mwilini kwa kuwa kiasi cha madini hayo kinachoondoka mwilini kwa njia ya mkojo ni kidogo sana.

“Hii ina maana kuwa, watu wenye maradhi ya figo wanatakiwa kuwa makini sana na kiasi cha madini ya potasiumu kinachongia mwilini mwao.

Pia Mboga za majani zitamsaidia mtu mwenye matatizo ya figo kwa sababu ina madini machache ya potasiumu.

(3) Wali mweupe

Chakula hicho kinashauriwa kutumiwa na watu wenye tatizo la figo kwa sababu mwili hatumii nguvu kubwa kukimeng’enya.

Nafaka nyingine zinazoweza kutumiwa ni pamoja na;

– shayiri,

– ngano na mahindi lakini kwa kiasi kidogo.

(4) Tunda la tufaha

Tunda la tufaha maarufu kama apple, ni miongoni mwa matunda ambayo mgonjwa wa figo anaweza kutumia kila siku katika mlo wake kutokana na kuwa na virutubisho ambavyo huisaidia figo kuondoa asidi.

– Matunda mengine ni pamoja na matunda ya jamii ya; zambarau, zabibu, balungi, nanasi, tikiti, na “strawberries”.

(5) Vyakula vyenye protini nyepesi

Ni muhimu kuepuka vyakula venye protini nyingi kwani metaboli ya protini huzidisha mabaki kama vile urea, amonia na “creatinine” ambayo tayari yako juu kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo na huleta madhara mwilini.

Inashauriwa kula protini ambazo zinatumiwa na mwili kwa ufanisi bila kuacha mabaki mengi.

Vyakula vyenye protini hizo ni pamoja na;

  •  mayai,
  • samaki,
  • nyama ya kuku,
  • maziwa na jibini.

(6) Vyakula vyenye kalori

Kwa mujibu wa Taasisi ya kimataifa ya Elimu ya Figo inabainisha kuwa mwili huhitaji kalori kwa shughuli za kila siku na pia kudumisha halijoto, ukuaji na uzito wa kutosha wa mwili.

Kalori hupatikana hasa kwenye kabohaidreti na mafuta na mahitaji ya kalori kwa wagonjwa wa figo ni 35-40 kcals/kg kwa uzito wa mwili kwa siku.

Kalori hupatikana kwenye vyakula vya  kabohaidreti kama;

– ngano (mkate), nafaka, mchele, viazi, ingawa wanashauriwa kutumia nafaka zisizokobolewa.

(7) Vyakula vyenye nyuzi nyuzi na visivyokobolewa husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula mwili.

“Vyakula vinavyowapa ulinzi ni vyakula vyenye madini ya alkali kama sodiam, potasiamu, magnesiamu, calsiamu na lisiamu.

Haya madini yanapatikana kwenye vyakula vya mboga mboga na matunda…..kwa hiyo kwa sababu hatuli vyakula hivi kwa wingi hivyo hivyo ile asidi  haitapoozwa na kuzidi kuongezeka mwishowe kuathiri figo,”

Asante kwa Kunielewa..!!!!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.