Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Wananchi zaidi ya 7000 Wafikiwa na Huduma za Uchunguzi na Matibabu ya Moyo

Wananchi zaidi ya 7000 wafikiwa na huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo kupitia huduma ya tiba mkoba ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge leo wakati akifungua kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayoendelea mkoani Kilimanjaro katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH).

Dkt. Kisenge alisema JKCI imekuwa ikifanya huduma ya tiba mkoba katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo hadi sasa mikoa 11 ya Tanzania bara na Zanzibar imeshafikiwa na wananchi takribani 700 kupewa rufaa kufika JKCI kwa ajili ya matibabu zaidi.
Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema kambi hiyo ya matibabu ya moyo ni muendelezo wa tiba mkoba ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services yenye nia ya kuwafikishia wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro huduma ya tiba bobezi ya magonjwa ya moyo mahali walipo.
“Nia ya JKCI kufanya kambi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi ni kuhakikisha kuwa tunaendeleza ujuzi kwa wataalamu wa afya wa hapa Mawenzi pamoja na kuwasaidia wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro ambao wana magonjwa ya moyo”,
“Mwitikio katika Mkoa huu wa Kilimanjaro umekuwa mkubwa sana ndani ya siku mbili tayari wagonjwa 600 wamefika katika Hospitali hii kwa ajili ya kupatiwa huduma, wagonjwa wengi wanaofika tumewakuta na shinikizo la damu na hii inatokea katika kila mkoa tunaoenda ugonjwa wa shinikizo la juu la damu umekuwa changamoto kwa watu wengi hivyo kupata madhara ya moyo kutanuka”,

Dkt. Kisenge alisema kuwa JKCI Itaendelea kufanya kambi hizo katika mikoa mingine iliyobaki lengo likiwa kuendeleza dhana ya kufikisha huduma za kibingwa kwa wananchi pale walipo.
“Katika kambi hii pia tunatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto ambapo kwa siku hizi mbili watoto waliofanyiwa uchunguzi wengi wao wamekutwa na matundu kwenye moyo”, alisema Dkt. Kisenge

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.