Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kupanda ngazi mara kwa mara hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo

Kupanda ngazi mara kwa mara hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo

Fahamu Utafiti mpya unaonyesha;Kupanda ngazi mara kwa mara kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kupata magonjwa ya Moyo,

Hii ni pamoja na kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ambapo  kwa kitaalam hujulikana kama “atherosclerotic cardiovascular diseases”, Pamoja na magonjwa mengine ya moyo na mishipa ya damu kwa ujumla yaani cardiovascular diseases (CVD).

Utafiti huo umegundua kuwa watu waliopanda ngazi 50 kwa muda wa siku walipunguza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu kwa asilimia 20% ikilinganishwa na watu ambao hawakupanda ngazi yoyote kila siku.

Ingawa utafiti ulilenga Ugonjwa wa moyo ambao hujulikana kama atherosclerotic cardiovascular disease (ASCVD)– unaojumuisha kiharusi, mshtuko wa moyo na kuganda kwa damu – hitimisho lake linatumika kwa magonjwa mengine ya moyo na mishipa ya damu kwa ujumla yaani cardiovascular diseases (CVD) kulingana na mwandishi wake.

Kumbuka: atherosclerotic cardiovascular disease (ASCVD)– hujumuisha magonjwa yanayoathiri moyo ikiwemo;

  • Ugonjwa wa kiharusi,
  • Tatizo la mshtuko wa moyo
  • Pamoja na tatizo la kuganda kwa damu

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.