Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Punguzeni kung’oa meno bali muongeze watu wanaotibiwa meno

Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wametakiwa kuhakikisha wanasimamia matibabu bora ya Kinywa na Meno na kupunguza kung’oa meno bali waongeze watu wanaotibiwa meno.

Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu amesema hayo leo Novemba 22, 2023 wakati akifungua Kongamano la 38 la kisayansi la Kitaifa na mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha wataalam wa Afya ya Kinywa na Meno linalofanyika Jijini Tanga.

“Mbali na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri lakini pia Hospitali zote za umma zinazotoa matibabu ya Kinywa na Meno zihakikishe zinaboresha miundombinu ya kliniki za Kinywa na Meno pamoja na kununua vifaa vya kisasa.” Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Takwimu za kuziba meno zimeongezeka kutoka asilimia 2 mwaka 2020 mpaka asilimia 36.1 mwaka  2023 ambapo hali hii imetokana na uwekezaji wa Serikali ya awamu Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Kuna Mikoa na Wilaya ambazo zimevuka 60%, nataka nione takwimu za kuziba meno zikiendelea kuongezeka na takwimu za kung’oa meno zikipungua, hali hii iende sambamba na utoaji wa elimu ya kinywa na meno kwa ajili ya kuzuia magonjwa yatokanayo na kukosa elimu sahihi ya kujikinga na magonjwa hayo.” Amesema Waziri Ummy.

Pia, Waziri Ummy amesema katika jitihada za Serikali za kuendelea kufanya mapinduzi Katika Sekta ya Afya imeweza kuajiri wataalam wa Kinywa na Meno 186 na kununua vifaa tiba vya kinywa na meno ikiwemo viti vya kutibia 55 vilivyokwenda kwenye Halmashauri 40 katika Mikoa yote nchini.

Amesema, Mwaka 2023/24 katika robo ya Kwanza na ya Pili ya mwaka jumla ya viti 207 vimeenda kwenye Halmashauri 160 vifaa tiba vya uchunguzi 82 zimeenda kwenye Halmashauri 70, na OPG mashine 1, CBCT mashine 1, gharama za Vitu vyote hivi ni zaidi ya TZS. Bilioni Saba.

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema Sambamba na uwekezaji huo, Serikali imeongeza ufadhili wa wataalam wa Sekta ya Afya hasa nafasi za kibingwa na ubingwa bobezi ndani na nje ya nchi kwa kutenga shilingi bilioni 8 ambapo kati ya hizo Tsh. Bil 3 zimetengwa kwa ajili ya kusomesha wataalam kwa seti ili kuleta ufanisi wakati wa utoaji huduma za kibingwa bobezi za Afya.

“Upande wa uzalishaji wa wataalam wa Kinywa na Meno vyuo vinavyozalisha Madaktari ngazi ya shahada vimeongezeka kufikia vitatu ambapo tunategemea hadi kufikia mwaka 2025 Tanzania itakuwa inazalisha zaidi ya Madaktari 100 wa Kinywa na Meno kwa mwaka kulinganisha na sasa ya wastani wa madaktari wanaozalishwa ni 40-60.” Amesema Waziri Ummy

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.