Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

jinsi ya kuongeza uume,fahamu ukweli wa mambo hapa

jinsi ya kuongeza uume,fahamu ukweli wa mambo hapa.

Swala la Kuongeza Uume imekuwa mada maarufu, huku wanaume wengi wakihitaji kujua jinsi ya kuongeza uume au maumbile yao na wengine hata kutumia vitu ambayo huwasababishia madhara makubwa sana kwenye miili yao,

Na hata wanaume wenye maumbile madogo wamekuwa wakiambiwa kuwa wana vibamia(kibamia-jina maarufu likimaanisha kuwa Mwanaume ana maumbile madogo au uume mdogo)

je ni kwanini Swala hili hutokea?

Swala hili hutokea kwa Sababu Wanaume wengi wana dhana kwamba wakiwa na Uume mkubwa au maumbile makubwa basi wataweza kufanya tendo la ndoa vizuri na kumfikisha mwanamke kileleni,

Wengine hupata ushawishi kwenye jamii zao kwamba,sifa ya Mwanaume ni kuwa na Uume mkubwa, wengine wanaamini wakiwa na maumbile makubwa wataonekana Rijali na watawavutia wanawake walionao.

Lakini pia Baadhi ya Wanawake wenyewe wanadhana hii, kwamba wakipata Wanaume wenye maumbile makubwa,basi italeta raha Zaidi kwao, hali ambayo huwafanya baadhi ya wanaume wenye maumbile madogo kutafta namna ya kuyaongeza ili kukidhi haja za wapenzi wao.

Fahamu Zaidi Kitaalam ikoje na nini unapaswa Kufanya kama Mwanaume;

Raha ya tendo la ndoa,Mwanamke kuridhika au kufika kileleni,Mwanamke kupata msisimko zaidi kwenye tendo n.k, vitu vyote hivi havitegemei ukubwa wa Maumbile yako,

Ili ufanikishe hili inategemea na ujuzi wako binafsi, kuufahamu vizuri mwili wa mwanamke ikiwemo sehemu zake za siri jinsi zilivyoumbwa, kwa kutumia akili na viungo vya mwili kuleta raha,kuongeza msisimko na kumridhisha mwenza wako.

Usichokijua ni kwamba;  Mwanaume unatakiwa kuwa na uume wa wastani kuliko mkubwa uliopitiliza unaoweza kusababisha maumivu kwa mtu unayeshiriki naye tendo,

Hali ambayo huweza kumfanya Mwanamke asifurahie tendo hilo na kuongeza uwezekano wa kupata hofu kutokana na ukubwa huo.

Hivo basi, Fahamu kwamba unaweza kuwa na Uume mkubwa na ukawa ndyo chanzo cha maumivu makali,michubuko,kupata magonjwa, na kuongeza hofu kwa mwenza wako ikiwa huna ujuzi wa jinsi ya kufanya mapenzi ili kumridhisha mwenza wako.

Mamlaka za ndani na kimataifa kama vile Wizara ya Afya, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na vyuo vikuu vilivyobobea kufanya utafiti kikiwemo chuo cha Havard, hakuna mahala ambapo wamepitisha na kupendekeza dawa au kifaatiba kwa ajili ya huduma hiyo ya Kuongeza maumbile au Uume.

Kitaalam: Hii inamaanisha swala sio kuhangaika na Size ya maumbile yako, Swala la msingi ni ujuzi wako binafsi, kuufahamu vizuri mwili wa mwanamke ikiwemo sehemu zake za siri jinsi zilivyoumbwa, kwa kutumia akili na viungo vya mwili kuleta raha,kuongeza msisimko na kumridhisha mwenza wako.

Fahamu maeneo muhimu ya kugusa wakati wa tendo la ndoa, hii italeta raha na kumfanya mwenza wako kuridhika Zaidi.

Watu wanene kupitiliza, shina la uume lililo chini ya kitovu humezwa na mafuta na nyama zilizorundikana hapo, hivyo kupunguza urefu wa kiungo hicho muhimu kwa tendo la ndoa,

Hivo kama ni mnene au Una Uzito mkubwa punguza uzito wako ili kuimarisha afya ya Uzazi ikiwemo nguvu zako za Kiume.

Zipo njia chache ambazo jumuiya za kimataifa na mamlaka za afya wanakubali kuwa zinaweza kusaidia angalau kuongeza urefu, lakini usiozidi nchi moja, njia hizo ni pamoja na kupunguza unene.

Hivyo, kupunguza unene kwa njia ya vyakula na mazoezi inakubalika. Vilevile kwa njia ya upasuaji kwa lengo la kupunguza mafuta ya eneo hilo inakubalika pia.

Tahadhari; Vitu vinavyotumika kiholela kunenepesha na kurefusha uume ni pamoja na vidonge, sindano, virutubisho, mashine maalumu, upasuaji wa kupandikiza, vifaa vya mazoezi ya uume, mafuta ya kupaka uumeni na mitishamba.

Vitu hivi vinauzwa kisiri katika baadhi ya maduka ya dawa, kwa njia ya mtandao, kutembezwa mtaani au matangazo kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari.

Lakini, kati ya hivyo nilivyotajwa, hakuna vinavyofanya kazi kwa ufanisi na kukidhi vigezo vya kitaalam kupitia vyombo vikubwa vya matibabu na uthibiti wa magonjwa ikiwemo WHO.

Kwa sababu hakuna utafiti wa kisayansi kuthibitisha ubora, ufanisi na usalama wa vifaatiba hivyo au njia zilizopendekezwa ingawa ni kweli, vipo baadhi ambavyo kwa muda mfupi, vinaweza kukusaidia lakini vikikuacha na madhara makubwa hapo baadaye.

Madhara hayo ni pamoja na;

  • kupungua au kukosa kabisa nguvu za kiume,
  • kuchubuka kwenye uume,
  • kuvunjika kwa misuli sponji ya uume,
  • madhara ya nerve
  • Pamoja na kupata maumivu sugu wakati wa kujamiana.

Taarifa zinaonyesha wanaume wengi hujikuta wakinasa na kununua vifaa hivi kwa sababu ya kuathirika kwao kisaikolojia ambako huongeza shauku iliyopitiliza ya kuongeza maumbile.

Ukidadisi unakuta wengi wao hawajawahi kwenda kwenye kituo cha huduma za afya au hospitali kwa ajili ya uchunguzi na ushauri. Wengi wanaojihisi wana uume mdogo hugundulika kuwa hawapo chini ya inchi tatu baada ya uume kusimama.

Chukua Tahadhari, jikinge na Madhara ya Muda Mrefu.!!!

Credits: #Dr.Ombeni Mkumbwa, #afyaclass, #Mwananchi, #WHO

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.