Mauaji yakatisha mechi ya ubelgiji na Sweden
Mchezo wa kuwania kufuzu mashindano ya Euro 2024 kati ya Ubelgiji na Sweden usiku wa kuamkia leo ulikatishwa wakati wa mapumziko kwa sababu za kiusalama baada ya raia wawili wa Sweden kuuawa kwa risasi jijini Brussels.
Mauaji hayo yalitokea saa chache kabla ya mchezo huo tukio ambalo limechukuliwa kama ugaidi.
Wachezaji na mashabiki walitakiwa kusalia ndani ya uwanja kwa zaidi ya saa moja baada ya mchezo kukatishwa kwa ajili ya usalama wao.
Timu ya Sweden imesema ilipata taarifa za mauaji hayo wakati wa mapumziko na ikakubaliana kwamba ni vema wasiendelee na mchezo kwa heshima ya watu hao waliouawa.
Bado haijafahamika kama waathirika hao walikuwa jijini Brussels kwa ajili ya kuangalia mchezo huo.