Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

jinsi ya kuzuia mimba siku za hatari

jinsi ya kuzuia mimba siku za hatari

Kuna njia kadhaa za kuzuia mimba siku za hatari, ikiwa ni pamoja na kutumia kondomu, vidonge vya uzazi, kalenda ya hedhi, na njia nyingine za uzazi wa mpango.

Ni muhimu kuzungumza na mtaalamu wa afya ili kupata ushauri unaofaa na kuchagua njia inayofaa kwa mahitaji yako na mwenza wako.

Njia nzuri ya jinsi ya kuzuia mimba siku za hatari ni ile ambayo hutumika kwa muda mrefu na huhusisha mzunguko mzima wa hedhi, kwa kitaalam tunaita long-acting form of contraception.

Njia ya kuzuia mimba ambayo unaitumia Siku za hatari pekee inaweza isiwe njia bora inayofanya kazi kwa asilimia 100%,

Kwani Mzunguko wako wa hedhi unaweza kubadilika muda wowote, kitu ambacho kitakuweka kwenye hatari Zaidi ya kupata Mimba, Ikiwa unazuia mimba kwa kuangalia Siku za hatari pekee.

Njia za Uzazi wa mpango zimegawanyika kwenye Makundi mbali mbali yakiwemo;

(1) Njia za kiasili(traditional methods)

Mfano; matumizi ya kalenda, Withdrawal method n.k

(2) Njia za kisasa(modern methods)

Mfano: Kitanzi, Vipandikizi, Sindano,Vidonge n.k

Pia tunaweza kuzigawanya kwenye makundi Zaidi kama vile;

  • Njia za muda mfupi
  • Njia za Muda Mrefu
  • Njia za kudumu

Soma Zaidi hapa Njia hizi za Uzazi wa mpango

jinsi ya kuzuia mimba siku za hatari

Zipo njia mbali mbali za Kuzuia Mimba ambazo unaweza kuzitumia ikiwemo;

1. Matumizi ya kitanzi au Lupu(IUD)

Soma Zaidi hapa kuhusu njia hii ya kutumia kitanzi(Intrauterine device)

#PICHA: Huu ndyo mfano wa kitanzi katika picha hii hapa chini;

2. Matumizi ya Kipandikizi au Kijiti

Njia jii huweza kuzuia mimba Siku za hatari na muda wake wa kuzuia mimba ni miaka 3 mpaka 5

  • Kuna kijiti cha miaka 3
  • Kuna vijiti vya miaka 5

Soma Zaidi hapa kuhusu njia ya vijiti au implants

3. Matumizi ya Sindano

Njia nyingine ya Kuzuia Mimba siku za hatari ni Sindano, Soma hapa faida na hasara za kutumia Sindano kama njia ya Uzazi wa mpango.

4. Njia nyingine za Kuzuia mimba Siku za hatari ni pamoja na;

Njia hizi za kuzuia mimba siku za hatari, kama vile kondomu, pia ni chaguo. Ingawa njia hizi hazina ufanisi zaidi kuliko hizo za juu. Bila shaka, utahitaji kutumia hizi kabla ya kujamiiana ikiwa hakuna namna.

Kumbuka: Ni muhimu sana kupata Maelekezo kwa kina kutoka kwa Wataalam wa afya Juu ya njia Sahihi ya kutumia ili kuzuia Mimba kulingana na mwili wako,

Hii itakusaidia kuzuia madhara ambayo huweza kujitokeza baada ya kuamua kutumia njia flani ya Uzazi wa mpango, au;

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.