Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ugonjwa wa kifua kikuu(tb),chanzo,dalili na matibabu yake(tuberculosis)

Ugonjwa wa kifua kikuu(tb),chanzo,dalili na matibabu yake(tuberculosis)

Katika Makala hii tumechambua Zaidi kuhusu Ugonjwa wa kifua kikuu(tb),chanzo,dalili na matibabu yake(tuberculosis).

Ugonjwa wa Kifua kikuu ambapo kwa kitaalam hujulikana kama TUBERCULOSIS(TB) ni ugonjwa wa kuambukiza ambao Huweza kumshambulia mtu yoyote na unaweza kuambukiza karibu kila sehemu ya mwili wa binadamu.

Kwa mujibu wa Takwimu za Shirika la afya Duniani(WHO);

Ugonjwa wa  Kifua kikuu cha mapafu maarufu kama TB ya mapafu ni miongoni mwa aina ya Ugonjwa wa kifua kikuu kinachoongoza kwa idadi kubwa ya visa duniani.

VISABABISHI VYA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)

Ugonjwa wa kifua kikuu au ugonjwa wa TB chanzo chake ni maaambukizi ya Bacteria,

Bakteria anayesababisha Ugonjwa wa kifua kikuu kwa kitaalam hujulikana kama mycobacterium tuberculosis.

Ugonjwa wa Kifua kikuu unaweza kuambukiza wanyama pia, na kifua kikuu cha ng’ombe kinaweza kupitishwa kwa wanadamu kupitia maziwa yaliyoambukizwa.  Utunzaji na ulaji unaweza kuwa chanzo cha maambukizo pia.

 ➖ Ugonjwa wa Kifua kikuu au ugonjwa wa TB kawaida huenea kwa njia Mbali mbali ikiwemo kupumua kwa matone yaliyoambukizwa yaliyosambaa hewani wakati mtu anapopiga chafya, kukohoa au kutema mate.

  Kutoka kwenye mapafu, bakteria wanaosababisha ugonjwa wa kifua kikuu(ugonjwa wa TB) Wanaweza kuenea sehemu zingine za mwili na kusababisha aina mbali mbali za ugonjwa wa kifua kikuu kama vile;

  • Ugonjwa wa kifua kikuu cha mifupa(Tb ya Mifupa),
  • Ugonjwa wa kifua kikuu cha ubongo(Tb ya Ubongo),
  • au ugonjwa wa kifua kikuu cha koo(Tb ya Koo) n.k. 

➖ Kuenea kwa bakteria ni polepole, kwa kweli kunaweza kuchukua muda wa miaka bila mtu kuonyesha dalili yoyote ya ugonjwa wa Kifua kikuu lakini ana vimelea Ndani ya mwili.

Sababu zozote zinazopelekea tatizo la  Kupungua kwa kinga ya mwili ndyo zitapelekea Mtu kuanza kuonyesha dalili za kuugua ugonjwa wa Kufua Kikuu au ugonjwa wa Tb mfano sababu kama vile;

  • mfadhaiko,Hofu,Msongo mkali wa mawazo,
  • au magonjwa mengine kama vile,UKIMWI,Ugonjwa wa Kisukari,saratani n.k

Hivi huweza kusababisha kinga ya mwili kuwa Dhaifu na Bacteria hawa wa Ugonjwa wa Kifua kikuu au ugonjwa wa Tb kuanza kusababisha dalili kujitokeza.  

Lakini pia Watu wanaoishi katika nyumba zilizojaa watu, wanaokaa maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu mara kwa mara,chakula duni na hali za chini sana huweza kushikwa na ugonjwa huu wa Kifua kikuu au Ugonjwa wa Tb.

Dalili za Ugonjwa wa Kifua Kikuu au Ugonjwa wa TB

 Dalili na Utambuzi wa ugonjwa wa kifua Kikuu(TB) Ni pamoja na;

 (1) Mtu Kupumua kwa shida sana

(2) Kupata kikohozi kinachoendelea, kinachoambatana na makohozi yenye damu

(3) Mtu kupata homa hasa homa za usiku Kuibuka.

(4)  Kuanza kupungua uzito kwa kasi,

(5) kupoteza rangi halisi ya Ngozi,

(6) mwili kukosa nguvu au kuwa dhaifu.

(7) Mwili kukonda sana baaada ya Kupata Ugonjwa wa kifua kikuu au TB

(8) Mwili kutoa sana Jasho hasa wakati wa Usku n.k

 Tiba ya ugonjwa wa kifua kikuu au Ugonjwa wa TB

 Ni muhimu sana kufanya Vipimo mara kwa mara,na endapo utagundulika Ugonjwa huu wa Kifua kikuu au Ugonjwa wa TB utaanza matibabu mara moja.

Hitimisho

Kuna Umuhimu mkubwa wa kuFahamu dalili mbali mbali za Ugonjwa wa Kifua kikuu au ugonjwa wa Tb ili kufanya vipimo mara moja pale tu ukiona haupo Sawa,

Dalili za ugonjwa wa kifua Kikuu au Ugonjwa wa TB Ni pamoja na;

(1) Mtu Kupumua kwa shida sana

(2) Kupata kikohozi kinachoendelea, kinachoambatana na makohozi yenye damu

(3) Mtu kupata homa hasa homa za usiku Kuibuka.

(4)  Kuanza kupungua uzito kwa kasi,

(5) kupoteza rangi halisi ya Ngozi,

(6) mwili kukosa nguvu au kuwa dhaifu.

(7) Mwili kukonda sana baaada ya Kupata Ugonjwa wa kifua kikuu au TB

(8) Mwili kutoa sana Jasho hasa wakati wa Usku n.k

Ukiona dalili kama hizi wahi Mapema Hospital kufanya vipimo.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.